GTranslate

Languages

Mayor's Message

"Ending AIDS means mobilizing more local resources, increasing investment in HIV prevention, through strong partnerships between public, private and community sectors."

Isaya Mwita Charles
Lord Mayor

Community Leadership Messages

“ Wanaume tumekuwa wagumu sana katika kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi na tukikutwa tuna maambukizi tunatakiwa tuanze kutumia dawa za kufubaza  kuliko kuwasubiri wenza wetu kwenda kupima na sisi ndo tupate majibu yetu kupitia wao”

 - Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuhakikisha inapamabana na UKIMWI  wameweka taratibu ya kila mwananchi anayepima maambukizi ya Ukimwi na akagundulika kuwa na virusi hivyo anaanza dawa za kufubaisha mara moja.

Kwa mujibu wake Dkt. Ndugulile amesema kuwa mpaka kufikia 2020 Serikali inataka kufikia malengo ya kimkakati ya 90 90 90 ambayo 90 ya kwanza inamaanisha watu wapime VVU  kufikia asilimia 90, 90 ya pili inamaanisha wanaopima VVU kama wana maambukizi waanze kutumia dawa za kufubaza na 90 ya tatu inamaanisha wenye VVU wawe wamefubaza ugonjwa huo.

Aidha Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa Watanzania wote kuchangia mfuko wa Udhamini wa kupamabana na Maambukizi ya Ukimwi kwa kupitia namba 0684909090 ili mradi kuweza kuongeza rasirimali fedha zitakazosaidia kwenye mapambano hayo.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya ukimwi Duniani ambayo huadhimishwa Decemba 1 kila mwaka watu wote wajitokeze kupima VVU.

Dr. Faustine Ndugulile
MD, MMed, MPH
Tanzania Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children

Thank You to our Donor